DIRA YETU AFRIKA NI NANI
Dira Yetu Afrika ni taasisi ya kijamii iliyoundwa na wajumbe kutoka wilaya ya Morogoro Mjini yenye dira ya Kuwa na jamii ya Kiafrika yenye maisha bora, maisha yanayopatiaka kutokana na Elimu, upatikanaji wa huduma za kibinadamu, uwekezaji na kuenzi uafrika. Kutokana dira hiyo sisi DIRA YETU AFRIKA tumedhamiria kuboresha maisha ya jamii za kiafrika kwa kufanya shughuli jumuishi, shughuli kama kutoa elimu, kujitolea kwa jamii, elimu ya ujasiriamali, elimu ya afya, kuandaa matamasha, shughuli za kiuchumi, kilimo na ufugaji. Kwa kufanya hivyo tunaamini tutaweza kuongeza kipato si tu cha mtu mmoja mmoja bali kuboresha maisha ya jamii nzima ya kiafrika. Hivyo kwa ufupi DIRA YETU AFRIKA inajihusiha na shughuli zilizo katika makundi yafuatayo
- Elimu na Afya
- Kilimobiashara
- Ujasiriamali na Uchumi
- Tehama, Ubunifu na Burudani & Michezo
Dhamira ya kikundi ni KUBORESHA MAISHA YA JAMII YA AFRIKA kwa kufanya shughuli jumuishi za kiuchumi na kijamii. Kwa kufanya hivyo tutaweza kuongeza kipato si tu cha mtu mmoja mmoja bali kuboresha maisha ya jamii nzima ya kiafrika. DIRA YETUAFRIKA – ni wewe ni mimi Tunafanikiwa kwa Kuwainua Wengine.
Tuna matamanio ya Kuwa na jamii ya Kiafrika yenye maisha bora, yanayopatikana kutokana na Elimu, upatikanaji wa huduma za kibinadamu, uwekezaji na kuenzi uafrika.
Tunapatikana Manispaa ya Morogoro Kata ya Mindu mtaa wa Kasanga Jirani na Kanisa Katoliki
DIRA YETU AFRIKA
Whatstapp: +255 776 441 991
E-mail: utawala@dirayetuafrika.com
Facebook: dirayetuafrika
Instagram: @dirayetuafrika
Twitter: @dirayetuafrika.com