DIRA YETU AFRIKA

Tunafanikiwa kwa Kuwainua Wengine

JINSI NILIVYONUSURIKA KUTEPELIWA NA MUUZAJI WA SIMU MTANDAONI

Wewe umeamua kunipigia simu kwa namba nyingine sasa ndio mambo gani hayo ya kubadilisha badilisha namba. Kama hutaki simu achana nayo. Alitamka hivo kisha akakata simu. Hakupokea tena simu kutoka kwenye namba zangu zote mbili. Namna hii ndio nilijua nilikua mbioni kutapeliwa na hawa wauzaji wa simu wa mitandaoni. Stori ilikuwaje? Najua unapenda stori mi pia napenda stori tena zile stori za matukio ya kweli. Eee waaa sasa mi ndio nipo hapa kukupigsha stori, stori zlie za kukuondolea stress na kukuelemisha pia. Kumbuka kuwa stori hizi ni mikasa na matukio ya kweli kabisa yaliwakumba watu tunaoishi nao kwenye jamii yetu. Ili stori inoge  nimechugua kutotaja majina yao. Wacha nisikuchoshe nikujuze ilikuwaje mpaka nikakaribia kutapeliwa na muuza simu wa mtandaoni.

Kama ilivyo kawaida Watanzania tulio upande wa bara tunaamina kabisa kuwa vitu hasa vile vitu vya kielectroniki  pamoja na magari vinauzwa bei nzuri sana upande wa Zanzibar bei ambayo kila mmoja anaweza kumudu kununua. Basi bwana nikiwa na mawazo hayo kichwani mwaka 2023 mwezi wa 6 nikabahatika kufika Zanzibar. Baada ya kukaa kwa muda kama wiki moja hivi nikapata pesa kiasi kadhaaa nikaamua nami nijibless kwa kununu smartphone maana muda huo nilikuwa natumia smartphone ya shemeji. Sasa bwana kwa kuwa mie sio mwenyeji sana mjini Zanzibar nikaamua niingie kwanza mtandaoni hasa instagram niangalia watu wanaotangaza kuwa wanauza simu. Nilidhani kuwa nitapata watu kadhaa kisha nitafanya mchujo kwa vigezo tofauti tofauti na wale nitakaopendezwa nao nitachuku namba zao na kuwapigia kabla ya kwenda dukani kwao.

Kumbe Zanzibari mambo ni tofauti kidogo na Tanzania Bara, Tz Bara watu wapo makini sana na kujitangaza kwenye mitandao ya kijamii yaani unakuta mtu muuza simu, au bidhaa nyingine yoyote halali anajitahidi sana kujitangaza kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook Twitter na kila namba ya Whatsapp ya mteja anayoipata anaisevu vizuri ili mteja huyo aweze kuona zile statasi za Whatsapp labda atavutiwa na bidhaa nyingine au hata kuwataarifu wengine kuhusu bidhaa za muuzaji huyo. Zanzibar bwana niliona ni tofauti kidogo wachache sana wanatumia kurasa na fursa za mtandao wa internet kujitangaza. Wengine wanakutajia majina ya kurasa zao ukitazama mara ya mwisho wamepakia maudhui ama kuposti chochote ni wiki 135 zilizopita yaani zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Ndio ivo basi katika wale niliona wapo siriazi ni pamoja na bwana mmoja yeye anajitangaza kuwa anauza simu zilizotumika ulaya na uarabuni lakini bado zipo katika hali nzuri kama mpya. Nilipitia matangazo yake kadhaa nikijiaminisha kuwa huyu anafaa hasa kwa kuwa kila siku anaweka matangazo kadhaa ya simu tofauti tena bei zake ni poa sana. Nikavutiwa na simu inaitwa SAMSUNG S8 PLUS. Kadiri ya tangazo lake alikuwa anaiuza laki moja na tisini. Basi bwana nilichukua namba zake nikampigia akanielewesha alipo, kuwa ni Zanzibar mjini kwenye jengo la Michenzani Mall. Kadiri tulivoongea alisistiza sana kuwa nitume pesa yaani laki moja na tisini na yeye angeweza kunitumia bila gharama ya ziada mpaka nyumbani kule mkoa wa kusni Unguja. Nilimkubalia na nikaonyesha kuwa kesho yake nitatuma pesa.

Kesho yake hata sikutuma pesa nilipanda gari niende mwenyewe nikalifahamu duka kwa macho yangu na nionane na yeye muuzaji maaana hii ni kama koneksheni si naweza kuanza kuchukua simu kwa huyu mwambana kuziuza kwa watu wengine au hata kupeleka Morogoro kwa ndugu zangu ili nami nipate faida kidogo. Cha ajabu huyu mwamba alipokea simu zangu zooote tangu nikiwa Kizimkazi mpaka nakaribia Kwerekwe lakini baada tu ya kufika kwenye lili jengo la Michenzani Mall akaacha kupokea simu zangu. Wakati mwingine nikipiga akawa anakata. Akili yangu nyingine yenye utulivu ikaniambia nimpigie kwa kutumia namba nyingine. Kweli nikafanya hivo akapokea vizuri tu, nami nikamkumbusha kuwa mie ndie yule mteja wake wa simu kutoka Kizimkazi na muda huo nipo Michenzani Mall lakini sijaliona duka lake basi anielekeze vizuri ili nifike tukafanye biashara. Alianza kufoka na kunilaumu kwa nini nampigia na namba mbili tofaauti na baada ya kufoka hivo akakata simu.

Hapo sasa nilibaki na mshangao na maswali lukuki. Kwani kumpigia simu kwa namba nyingine ni kosa? Lakini si ni yeye ambaye hataki kupokea simu yangu kwa namba yangu ya awali? Au huyu mtu hana duka hapa michenzani Mall?  Au ni ana simu mbili tu mfukoni kakwapua sehemu fulani anakuja kuuzia hapa.? Au ni tapeli? Maswali yakawa mengi na mengine zaidi tena yasiyo na majibu.

Nikajaribu kuurudia ule ukurasa wake wa instagram nikagundua kuwa simu zake zote mara zote bei huwa ni chini kuliko wauzaji wengine, pia yeye hajawahi kuweka picha ya tangazo ikiwa imepigwa ofisini kwake, pia hajawahi kuweka sura yake. Hapo akili ikashtuka. Kumbe yeye alitegemea mie ningetuma pesa ili anitapeli huku akijisifu kuwa wanatuma mikoa yote kwa uaminifu kabisa. Sasa kwanini hakutaka tuonane?

Basi nilijaribu kuzunguka zunguka mule Michenzani Mall nikitazama kila duka kwa umakini labda nitaona duka la yule bwana wapi. Sikuona duka lake wala matangazo yake nje ya mlango wowote. Niliyaona maduka ya watu walio makini kwenye biashara kama Biggie Electronics na wengineo. Tangu siku hiyo nilifuta namba yake ya simu na kuacha kabisa kumfuatilia kwenye ukurasa wake wa instagram. Nikaenda zangu eneo la darajana kwa dada mmoja nae akaniuza simu kama ile kwa kwa shilingi lakini mbili na themanini. Kwa leo tuishie hapa.

Nakukumbusha pia kuwa uhuru wako unaishia pale uhuru wa mwingine unapoanzia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *